• HOME
  • NEWS
  • ABOUT US
  • ZONAL ATTRACTIONS
    • Lake Zone
    • Southern Zone
    • Eastern & Coastal Zones
    • Central Zone
    • Northern Zone
  • CULTURAL TOURISM PROGRAMMES
  • JOBS AND SCHOLARSHIP
  • ANNOTED ATTRACTIONS
You are here : Home »
Showing posts with label Entertainment. Show all posts


 Mratibu wa Shindano la Miss Dar Intercollege 2012, Dina Ismail akiwanadi warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 wakati wa uzinduzi wa bendi ya SkyLight ndani ya Mafian Lounge jijini Dar es Salaam wikendi iliyopita.
 Warembo wakionesha umahiri wao wa kupita jukwani.
 Warembo wakionesha umahiri wao wa kupita jukwani.
 Wakipita wa mwendo wa twiga.
 Wakifunguliwa shampeni kwa nderemo na vifijo.

Baadhi ya Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiwamejipanga mbele ya wadau na wadhamini katika uzinduzi wa bendi ya SkyLight iliyofanyika  Mafian Lounge iliyopo Masaki, bendi hiyo inamilikiwa na mmoja wa wadhamini wao Ndege Insurance.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
Alisema mpaka sasa warembo 15 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus, Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.
Diamond  mapema leo akiwa katika studio za Clouds FM kwa ajili ya interview.
---


Kwenye kipindi cha XXL leo kinacho rushwa na Clouds Fm msanii Diamond aliulizwa ni kwa vipi aliweza kujielezea vizuri sana kwa lugha ya Kingereza baada ya performance yake kwenye Big Brother StarGame maana wengi huwa wanashindwa ifikapo hatua hiyo Diamond alifunguka na kukiri kwamba mrembo Wema Sepetu amechangia kiasi kikubwa kwake kujua lugha hiyo na kusema napenda kumshukuru 'WEMA ENGLISH COURSE'...... kusema ukweli nilifurahi sana kusikia hivyo maana pamoja na mascandal yao yote angalau Diamond ameweza kuongelea upande mzuri wa Wema na ni jinisi gani ameweza kuchangia mafanikio yake kwa kiasi flani.

Wakati huo huo Diamond pia ameongela tour yake ambayo anatarajia kuifanya nchini Marekani baadae mwaka huu na nyumba anyo jenga Tegeta ambayo amekiri mpaka sasa ametumia karibia Tshs milioni 69. Nyumba ni ya kisasa, ina vyumba vya kulala vinne, vitatu vyote master, kuna studio, jiko, choo, bafu nk. Pamoja na nyumba hiyo kuna zingine pia ambazo hakupenda kuongelea ila I hope and I'm sure kuna siku atafunguka.

Tunapenda kumtakia kila la kheri Diamond na Big Up to mrembo Wema Sepetu kwa msaada alio mpatia Diamond kwa kumfundisha Kingereza.
RAIS wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki na Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino Mokiwa amesema waumini Wakristo hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi ukiwemo ufuatiliaji wa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha viongozi wa Dini na Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais jana, Dk Mokiwa alisema Polisi imeshindwa kufuatilia matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa makanisa hayo.

Alisema tangu mwaka jana zaidi ya makanisa 25 yamechomwa moto na hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani.

“Matukio mengi ya kuchomwa moto kwa makanisa yamejitokeza Zanzibar tangu mwaka jana lakini hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani au mtu aliyekamatwa,” alisema Dk Mokiwa.

Aidha, alisema hadi sasa wafuasi Wakristo wanafanya kazi zao kwa hofu na wasiwasi kwani baadhi ya watu bado wanashambulia nyumba za ibada ikiwa ni pamoja na kurusha mawe.

“Hadi sasa wafuasi wetu wanafanya kazi zao kwa wasiwasi mkubwa hata katika nyumba za ibada kwani wafuasi wenye siasa kali wanarusha mawe katika nyumba za ibada,” alisema.

Dk Mokiwa alisema hakubaliani na kauli za baadhi ya watu kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni wahuni, bila hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Alifafanua, kuwa kama ni suala la Muungano kwa nini watu hao wachome moto makanisa na wasisubiri Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba ili wawasilishe hoja zao kuhusu Muungano.

“Sisi hadi sasa hatuamini kwamba wanaofanya fujo ni wahuni, kama ni wahuni kwa nini wanachoma moto makanisa na kama ni Muungano kwa nini wasisubiri Tume ya Katiba? “Alihoji Askofu Mokiwa.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akijibu baadhi ya hoja za Baraza la Maaskofu Tanzania, alisema tayari Serikali imeweka ulinzi wa kutosha kwa makanisa yote visiwani hapa.

“Tumeweka ulinzi katika sehemu zote za nyumba za ibada ikiwamo makanisani na Serikali itahakikisha hakuna fujo zitakazojitokeza kwa sasa,” alisema Aboud.

Aliahidi kuwasilisha kwa Rais Dk Ali Mohamed Shein malalamiko yao yote kuhusu vitendo vya kuwadhalilisha Wakristo visiwani huku Tanzania ikiwa nchi isiyo na dini isipokuwa wananchi.

Mapema viongozi hao walitaka kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) kuzungumzia matukio hayo yenye kuashiria uvunjifu wa amani na utulivu.

Hata hivyo Aboud alikiri akisema wapo watu wanatumia vibaya taasisi za kidini kama mwamvuli wa kisiasa katika kuwasilisha hoja zao mbalimbali, yakiwamo masuala ya Muungano na marekebisho ya Katiba.


JULIO

Age27
Country
Tanzania
OccupationManager
BiographyJulio is from Dar es Salaam and works as the Head of VAS, Electronic Channels and Products at a company in the telecommunications industry. With a BComm in Finance and an MBA under his belt, he looks set to be a wily player on Big Brother StarGame! He entered to be on the show because his best friend – Hilda – was the perfect example of the best candidate. Coupled with that, he saw himself as the most complete character because of how he lives his life as a hedonist.

He says of his partner Hilda that she is “real and straightforward” and that he’s always comfortable when she’s around. He says that men adore her while women are always on his case. “She’s smart, very interesting – especially with how much she knows, Africa will love her to death,” he says. He’s a fan of the show and cites Kevin as his favourite Housemate, though he says “at the end of the day, he has nothing on what I’ll bring to the House”. 

Julio describes himself as fun, crazy, smart, cunning and entertaining.
 

HILDA

Age28
Country
Tanzania
OccupationSaleswoman
BiographyHilda hails from Morogoro and is a saleswoman. She has a son and enjoys the novels of Sydney Sheldon and the book Memoirs of a Geisha. Hilda was inspired to enter Big Brother StarGame by Biggie himself! “He seems to be a big challenge in the House and so I thought it would be fun to join him this time around and give him a special challenge. I can’t wait…” she says. She’s excited by the partnering format of this year’s show as it will be filled with fun and entertainment – plus her partner Julio is her best friend. “He is charming, sweet and a very good listener, of course,” she says.

She says she will do whatever it takes to win the grand prize – including lying her way out of a tricky situation or “being the sweetest thing ever”. She knows that Africa will be talking about her as soon as they see her on screen – which makes her excited. She says if she wins, she will donate money to a charity she supports back home as a peer health educator to help them build a nice house


SOURCE: bigbrotherafrica.dstv.com
Next Home
ADVERTISMENT
Sanya Consultant Company; deals with project proposal writing, conducting ESIA in different projects, research proposal writing.

contact: +255789606882

LISTEN RADIO FREE AFRICA LIVE

Most viewed Contents

  • TCU Guide book - Kwa wanaoomba vyuo 2012/2013
  • Engaruka:Kabila lililotoweka kimiujiza
  • WASHIRIKI WA BIG BROTHER FROM TANZANIA HAWA HAPA
  • Mbeya
  • Mamba / Marangu
  • MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA 2012/2013
  • MAIGE: "NAPE NI GAMBA"
  • DIAMOND: "NAMSHUKURU WEMA SEPETU KWA KUNIFUNDISHA KIINGEREZA"
  • Boma la Mjerumani Mikindani ni kivutio
  • Bujora Museum

Utalii Tanzania On facebook

football online

Footbal Updates

Get Adobe Flash player
live scores

Online Visiters

© 2012 - Utalii Tanzania. All rights reserved.

Designed by Mhoja L. Matandiko

hit counter