• HOME
  • NEWS
  • ABOUT US
  • ZONAL ATTRACTIONS
    • Lake Zone
    • Southern Zone
    • Eastern & Coastal Zones
    • Central Zone
    • Northern Zone
  • CULTURAL TOURISM PROGRAMMES
  • JOBS AND SCHOLARSHIP
  • ANNOTED ATTRACTIONS
You are here : Home »
Showing posts with label sports. Show all posts
Vicente del Bosque 

Del Bosque the man, the manager


Coach Vicente del Bosque has hailed Spain's "great generation of footballers" after their historic win over Italy in the final of Euro 2012.
La Roja's 4-0 victory in Kiev made them the first team to win three successive major international tournaments.
"We're talking about a great generation of footballers," said Del Bosque.
"They know how to play together because they come from a country where they learn to play properly. This is a great era for Spanish football."
  • Vicente del Bosque was born two days before Christmas 1950.
  • His hometown is Salamanca in western Spain.
  • Played as a midfielder for Real Madrid for 14 years, winning five league titles and four cups.
  • Represented Spain 18 times between 1975-80.
  • Had three spells in charge of Real, winning the league and the Champions League twice.
  • Del Bosque has managed the national side since July 2008.
  • He is only the second coach to win a European Championship and a World Cup, joining Helmut Schoen of West Germany.
The 61-year-old added: "We have some great lads who play abroad, which was impossible before. We didn't really have players abroad and now foreign clubs want our players.
"To win three titles is almost impossible. Congratulations to the players.
"It's true we were lucky enough to play a great match. Everything worked for us. It was an extraordinary performance against a difficult opponent.
"We played our own game. There were no real external influences - we were faithful to what we've done in recent years.
"I didn't really want to be the coach who wins but the coach who educates. I want to keep preparing them for the future."
Spain were at their scintillating best as goals from David Silva, Jordi Alba, Fernando Torres - who became the first player to score in two Euros finals - and Juan Mata helped them overpower the Italians by the biggest winning margin in a Euros final. They also retained the crown they first won in Vienna four years ago.
Between these two, La Roja have also claimed their first World title in South Africa and have now constructed a compelling case to be classed as the best team in history.
Sunday's victory was also the perfect riposte to the critics who have suggested that Spain have abandoned attacking principles and are not entertaining to watch.
Spain midfielder Cesc Fabregas told BBC Sport: "It feels really, really amazing. It's one of the best days of my life.
"I don't think we realise what we've done. In time we'll see. Are we boring? People who think we are boring, I don't think they understand the game."
Spain captain Iker Casillas, for whom Sunday's win was his 100th from 137 caps said: "There will always be some criticism as we have set the bar so high. That's what happens when you come down a step. It's been four marvellous years.
"You might think that a 4-0 margin against Italy means it was easy - but we have been gradually stepping up as the tournament went along.

KOCHA wa timu ya Simba Mserbia, Milovan Cirkovic, amesema anataraji kikosi chake kitafanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu kwani kwa sasa anaelekeza nguvu zote kwenye ligi msimu ujao.

Akizungumza jijini juzi kwenye Viwanja vya Sigara Chang'ombe ambako timu hiyo inapiga 'tizi', alisema kuwa mkazo wake zaidi ni kwenye ligi kwa kuwa Kombe la Kagame ni mashindano ya wiki mbili tu.

"Nitaingia kwenye Kagame kwa lengo la kusaka ubingwa, lakini nguvu nyingi nitazielekeza kwenye Ligi Kuu ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kimataifa.

"Unajua nikifanya vibaya kwenye ligi siwezi kupata nafasi ya kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho Afrika ndiyo maana naelekeza nguvu zangu kwenye ligi zaidi."

Kuhusiana na hali ya mazoezi inavyoendelea Milovan alisema wachezaji wake hadi sasa wanaonekana kuelewana kiasi kwamba ana matumaini ya kufanya vizuri katika michezo iliyo mbele yao.

Alisema beki mpya wa klabu hiyo Masombo Lino, kutoka DC Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anaimudu vema nafasi yake hiyo na kufanya wasiwasi kuhusu Kelvin Yondan umtoke.

"Wachezaji wapo vizuri nimependa wanavyofanya mazoezi kwa kuelewana na nilikuwa nina wasiwasi na nafasi ya Kelvin Yondan ambaye hayupo lakini huyu kutoka Motema Pembe ameiziba na anamudu vema kuzuia na kusaidia mashambulizi pia" alisema.
xxx
Katika hatua nyingine kocha huyo atawakosa nyota wake beki Kelvin Yondani na kipa Ally Mustapha 'Barthez' waliojiunga na Yanga, winga Salum Machaku alipelekwa Mtibwa Sugar.

Beki raia wa Uganda, Derick Walulya, mshambuliaji Jamhuri ya Afrika Kati, Gervais Kago wameachwa.

Beki mwingine ambaye ametangazwa kuachwa ni Juma Jabu na Salum Kanoni ambaye hata hivyo, mkataba wake umebakisha siku mbili kumalizika.

Wachezaji ambao klabu hiyo inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Haruna Shamte na Shija Mkina. Mkina bado anacheza kwa mkopo Kagera Sugar.
Cristiano Ronaldo 
Cristiano Ronaldo's goal in the 79th minute gave Portugal a 1-0 win over the Czech Republic in the first Euro 2012 quarter-final on Thursday.
Portugal will face the winner of Saturday's Spain-France match in the semi-final.
The two sides played to a scoreless first half with Portugal coming closest to scoring when Ronaldo hit the post after a fine piece of skill at the end of the opening 45 minutes.
Both sides enjoyed bright moments, with the Czechs prompted by the lively Petr Jiracek and Portugal looking to release their dangerous captain Ronaldo at every opportunity.
The winger failed to connect cleanly with an overhead kick to the delight of the Czech fans and fired a powerful 35-metre free kick well wide but almost scored after turning brilliantly before planting a firm shot against the post from a tight angle.
Nani and Miguel Veloso were booked for over-zealous tackles as tempers flared in a humid atmosphere under the closed roof at the National Stadium and the Portuguese suffered another blow when striker Helder Postiga was forced off with an injury.
Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omori akijaribu kutaka kuwatoka mabeki wa Ethiopia wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake uliofanyika kwenye Uwanja wa Tanifa jijini Dar es Salaam. Ethiopia imeshinda 1-0 na kuitoa mashindanoni timu ya Tanzania.
Wachezaji wa Ethiopia pamoja na viongozi wao katika benchi la ufundi wakifurahia ushindi wa timu yao
Ubao wa Matokeo
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema atamwanzisha beki Erasto Nyoni kuziba pengo la Aggrey Morris katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Gambia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nahodha huyo msaidizi wa Stars, Morris ataikosa mechi hiyo ya Jumapili kwa sababu anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Ivory Coast wiki iliyopita ambao pia ulikuwa wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil 2014.

Kim alisema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jana asubuhi ya kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume.

“Aggrey (Morris) hatakuwepo kwenye mchezo wa Gambia, anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Ivory Coast, lakini nitamwanzisha Nyoni kucheza nafasi yake,” alisema Kim.

“Nilimwona anavyocheza dakika chache kwenye mchezo wa Ivory Coast, alicheza vizuri na kwa utulivu, ni mchezaji mzoefu na anajua jinsi ya kumdhibiti adui.”

Alisema, "hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi, nafikiri hakutakuwapo na sura mpya zaidi ya wale waliocheza mchezo uliopita na Ivory Coast."

"Nafikiri itawasaidia kuelewana na kucheza kwa mpangilio ulio sahihi, nafahamu kila mmoja wetu anataka kuona tunaifunga Gambia," alisema Kim.

Aliongeza kuwa hana wasiwasi kukosena kwa Morris kwani anawaamini wachezaji wote aliowaita kwenye kikosi hicho kwamba ni wazuri na wenye kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.

“Kila namba nilijaribu kuita wachezaji wawili, nilifahamu inaweza kutokea mmoja ameumia au kutumikia adhabu ya kadi, nafikiri yote yametukuta, lakini tunasonga mbele," alisisitiza Kim.

Kocha huyo amemwondoa kwenye kikosi hicho beki wa Simba, Masoud Nassoro 'Chollo' kutokana na kuumia goti.

Daktari wa timu hiyo Mwanandi Mwankemwa alisema, "uchunguzi unaonyesha tatizo hilo ni la muda mrefu kwa Chollo, alijitonyesha, atachukua muda kidogo kurudi katika hali yake ya kawaida."

Wachezaji wengine ambao walikuwa majeruhi, lakini wamejiunga na wenzao na kufanya mazoezi ni viungo, Haruna Moshi 'Boban' na Nurdin Bakari.

Wakati huohuo; mtaalamu wa tiba ya viungo wa klabu ya Azam FC, Paulo Gomez amejitolea kuwafanyisha mazoezi maalumu Haruna Boban' na Nurdin ili warejee kwenye kikosi cha Stars haraka.

Boban, Bakari, Said Nassoro 'Cholo'na Thomas Ulimwengu  hawakujumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoikabili Ivory Coast ugenini kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Mmoja wa viongozi wa bechi la ufundi la Taifa Stars aliliambia Mwananchi kuwa Gomez pia ndiye alichunguza afya za wachezaji wote wa timu hiyo siku mmoja kabla ya safari ya Ivory Coast na kubaini matatizo kwa Boban na Cholo yaliyosababisha  kuondolewa kwao.

Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kumaliza programu yake ya mazoezi na wachezaji hao kwenye Uwanja wa Karume, Gomez alisema anafanya kazi hiyo bila malipo yoyote kutokana na mapenzi yake kwa Tanzania.

"Mimi ni mtaalamu wa tiba za viungo, TFF iliniomba nije niwasaidie na mimi nilikubali kwa moyo mmoja.

"Hapa nilipo najitolea tu silipwi chochote na mimi naridhika kwa sababu napenda kuisaidia Tanzania,"alisema Gomez.

Gomez alisema kuwa mazoezi anayowapa Boban na Bakar yana lengo ya kumaliza maumivu na kuwarejesha katika hali ya kawaida.

"Mazoezi haya yanachukua dakika 45 mpaka saa moja, ni aina ya mazoezi ambayo lengo lake ni  kumwezesha majeruhi kurejea katika hali ya kawaida,"alisema Gomez.  source: mwananchi.co.tz

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam wakati alipotangaza zawadi kwa washindi wa tuzo za mwanamichezo bora zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA, kulia ni  Amir Mhando Katibu mkuu wa TASWA na katikati ni Juma Pinto Mwenyekiti wa TASWA.

(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI)

MWANAMICHEZO Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 anatarajiwa kupewa dola za Marekani 8,000 (Zaidi ya sh. Milioni 12 za Tanzania).Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Imani Lwinga alisema uamuzi wa kutoa fedha una lengo la kumpa uhuru mshindi aweze kufanya mambo anayoyapenda kutokana na zawadi hiyo.
 
“Nia ya kutoa zawadi ni kumfanya mshindi aone ana kitu fulani amepata, hivyo safari hii tumeona tutoe kiasi hicho cha fedha ambacho tunaamini kitakuwa changamoto kubwa kwa mshindi,” alisema Lwinga.Alieleza kuwa walipokea ombi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambacho ndiyo kinaandaa tuzo hiyo, kwamba safari hii kuwe na mabadiliko kwa mshindi akabidhiwe fedha badala ya zawadi ya gari kama ilivyokuwa mwaka jana. Pia mshindi huyo wa jumla atapewa cheti na kombe.
 
Lwinga alisema pia Serengti itatoa zawadi ya Sh. Milioni moja kwa kila mshindi wa michezo mbalimbali ambayo itazawadiwa katika sherehe hizo zitakazofanyika Juni 14 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
 
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema wanatarajia wanamichezo mbalimbali watapewa tuzo siku hiyo na kutaja michezo ambayo itapewa tuzo kuwa ni riadha, wavu,netiboli,kuogelea, tenisi, judo, kikapu, soka, ngumi  za kulipwa, ngumi za ridhaa,  gofu wa ridhaa, gofu wa kulipwa, baiskeli, kriketi.
 
Mingine ni mpira wa mikono, olimpiki maalum, Mchezaji Bora wa Nje anayecheza Tanzania, Mchezaji Bora Chipukizi, Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza Nje, Karate, Mwanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2011 na  Tuzo ya Heshima.
 
Mhando ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Tuzo alisema Ijumaa watatangaza majina ya wanamichezo wote watakaowania tuzo hiyo na kuipongeza Serengeti kwa udhamini wao wa kila mwaka.
 
Kwa mujibu wa Mhando mwaka 2006 Mwanamichezo Bora wa Tanzania alikuwa Samson Ramadhan aliyezawadiwa sh. 500,000, wakati mwaka uliofuata mshindi ambaye alikuwa Martine Sulle alizawadiwa Sh.500,000, huku mwaka 2008 mshindi akiwa Mary Naali alizawadiwa sh.750,000. Wote hao ni wanariadha.
 
Mshindi wa mwaka 2009 alikuwa mchezaji netiboli Mwanaid Hassan aliyezawadiwa sh. Milioni moja na mwaka 2010 pia alikuwa Mwanaid aliyezawadiwa gari aina ya Toyota Cresta GX 100 .
 
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa  TASWA, Juma Pinto aliwashukuru Serengeti na kusema kuwa ana matumaini zawadi hizo itakuwa kichocheo cha wanamichezo kufanya vizuri zaidi.


Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter  Msigwa na  Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011  waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
 (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)
Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.
Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani. 
Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.
Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao
Luis Moreno Ocampo

Mwanasheria mkuu wa Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza kesi za makosa ya jinai, Luis Moreno Ocampo ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Mkuu wa kundi la upelelezi kwenye makao makuu ya FIFA. Msemaji wa mwenyekiti wa Kamati ya utawala huru ya FIFA, Mark Pieth, amethibitisha habari kuwa raia huyo wa Argentina ni miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo, ikiwa ni sehemu ya wimbi la mageuzi yenye lengo la kukabiliana na rushwa pamoja na ufisadi.

Pieth, ambaye ana sifa ya kua mtaalamu wa masuala ya utawala, ndiye anayewajibika na kuwazsilisha orodha ya wagombea wanaostahili kwa kamati kuu ya FIFA. Wanachama wa Shirikisho walikubaliana kwa kura mjini Budapest wiki iliyopita kuunda tume ya nidhamu, pamoja na uchunguzi wa kina na pia afisi ya maamuzi.
Watakashinda nafasi hizo watatangazwa tarehe 29 Juni.
fifa
Mageuzi haya yalipendekezwa baada ya madai upendeleo na rushwa kutumika katika kupanga mashindano ya Kombe la dunia la mwaka 2022 katika Taifa la Ghuba la Qatar.
Image

MWENYEKITI wa Yanga, Lloyd Nchunga ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kuanzia jana.

Kujiuzulu kwa Nchunga itakuwa furaha kwa Baraza la Wazee la Yanga, ambalo karibu mwezi mzima sasa limekuwa likimshikia bango Nchunga aachie madaraka kwa madai ya timu hiyo kufanya vibaya katika Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika mapema mwezi huu, ambapo Yanga ilishika nafasi ya tatu.

Pia itakuwa imewarahisishia kazi baadhi ya wanachama wa Yanga, ambao walikutana makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na kutangaza kumpindua Nchunga, uamuzi ambao ulipingwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba ni kinyume cha Katiba.

Uamuzi huo wa Nchunga kujiuzulu aliutangaza jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake jengo la NSSF, Dar es Salaam na kwamba amefanya hivyo kwa maslahi ya Yanga.

Alisema uamuzi wake wa kujiuzulu umekuja wakati walishakubaliana kwenye kikao cha
Kamati ya Utendaji ya Yanga kwamba wajumbe wengine waliobaki wasijiuzulu hadi mkutano mkuu wa wanachama Julai 15 mwaka huu, lakini mazingira yamemfanya afikie uamuzi huo na kwamba anajua wenzake watasononeka sana.
more information; http://www.habarileo.co.tz/michezo

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.


Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.


Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
- Habari na Issa Michuzi blog

Na Ezekiel Kamwaga, Khartoum

*Walishwa lunch saa 10 jioni
*Chakula cha usiku saa sita usiku
*Rage, Kisaka, wanyimwa pa kulala, walala mapokezi
* Wachezaji wajifua kivyao

UONGOZI wa Simba SC unakusudia kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na unyama inaofanyiwa nchini Sudan inakosubiri pambano lake dhidi ya Al Ahly Shendi kesho.
Tangu iwasili nchini Sudan juzi, Simba imekuwa ikifanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na wenyeji wake, Shirikisho la Soka Sudan (SAF) na Al Ahly Shendi.

Jana, Simba ilifanyiwa vitendo hivyo kabla ya kwenda katika mji wa Shendi itakakochezwa mechi hiyo na baada ya kufika katika mji huo uliopo takribani kilomita 170 kutoka mji mkuu Khartoum.

Simba iliwasili Shendi majira ya saa mbili usiku kwa saa za Sudan (sawa na saa za huko) baada ya safari ya takribani masaa manne kutoka Khartoum.

Safari ya kutoka Khartoum hadi Shendi ilianza majira ya saa kumi jioni na timu ikafika saa mbili usiku, kwa maana ya masaa manne ya safari ya barabara jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za CAF zinazozungumzia umbali usiozidi masaa mawili.
Ingawa kanuni ya CAF kifungu cha 5 (3) kinazungumzia umbali wa kusafiri kwa basi usizidi kilomita 200, Simba inaweza kutuma malalamiko kwamba kutoka Khartoum hadi Shendi ni zaidi ya kilomita 150 kwa vile si haiwezekani kutumia masaa manne kwa umbali huo.

VITUO LIGI YA TAIFA VYAPANGWA
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga vituo vitatu vya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa kwa ajili ya ligi hiyo itakayoanza Mei 26 mwaka huu.

Kundi A lenye mabingwa wa mikoa ya Iringa (Kurugenzi Mufindi), Lindi (Lindi SC), Mbeya (Tenende FC), Morogoro (Mkamba Rangers), Mtwara (Ndanda SC), Pwani (Super Star), Rukwa (Mpanda Stars) na Ruvuma (Mighty Elephant) zitacheza mechi zake mjini Mtwara.

Mji wa Kigoma utakuwa mwenyeji wa mabingwa wa mikoa ya Dodoma (CDA), Kagera (Bandari FC), Kigoma (JKT Kanembwa), Mwanza (Pamba SC), Shinyanga (Mwadui SC), Singida (Aston Villa) na Tabora (Majimaji).

Kundi C lenye mabingwa wa mikoa ya Arusha (Flamingo SC), Dar es Salaam (Ashanti United ya Ilala, Red Coast ya Kinondoni na Tessema FC ya Temeke), Kilimanjaro (Forest FC), Manyara (Nangwa VTC), Mara (Polisi Mara) na Tanga (Korogwe United) watachezea mechi zao mkoani Mara.

Mwisho wa kuwasilisha fomu za usajili ni Mei 15 mwaka huu wakati kipindi cha pingamizi ni kuanzia Mei 16 hadi 22 mwaka huu. Mei 23 mwaka huu Kamati ya Mashindano ya TFF itakutana kupitia usajili huo. Wachezaji wanaosajiliwa ni wale wale waliochezea timu hizo katika ligi ya mkoa.

Mei 14 mwaka huu ni mwisho kwa mikoa yenye pingamizi kwa mabingwa wao kuwa wameshashughulikia rufani husika. Kamati ya Mashindano imeagiza kuwa kwa mikoa itakayoshindwa kufanya hivyo mpaka baada ya tarehe hiyo mabingwa wao hawatashiriki ligi hiyo.

Timu tano zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi na washindwa wawili bora (best losers) kutoka kundi A na C ambayo yana timu nane kila moja.

LIUNDA KUSIMAMIA MECHI LESOTHO
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2014 Kanda ya Afrika kati ya Lesotho na Sudan itakayochezwa jijini Maseru.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa kati ya Juni 1 na 3 mwaka huu. Lesotho na Sudan ziko kundi D pamoja na Ghana na Zambia.

Naye Hafidhi Ally ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Kamishna wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Dynamos FC ya Zimbabwe na Esperance Sportive ya Tunisia.

Mechi hiyo ya marudiano hatua ya 16 bora itachezwa Mei 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa Rufaro jijini Harare. Esperance Sportive ilishinda mechi ya kwanza kwa mabao 6-0.
Chelsea wamechukua ubingwa wa Kombe la FA Cup kwa mara ya saba, kufuatia magoli kutoka kwa Ramires na Didier Drogba dhidi ya Liverpool. Ramires alifunga kufuatia kosa la Jay Spearing, kabla ya Didier Drogba kufanikiwa kumkwepa Martin Skrtel na kuandikisha bao la pili.

Liverpool walionyesha mchezo duni hadi Andy Carroll alipofunga bao moja baada ya John Terry kukosa kuimarisha ngome ya Chelsea kikamilifu, na mabao kuwa ni magoli 2-1.

Kulikuwa na ubishi kwa muda uwanjani baada ya Carroll kudhani alikuwa amefunga bao la kusawazisha kwa kichwa, na Petr Cech kuutema mpira huo, ambao kwanza uligonga mwamba na kuanguka mbele ya msitari. Wachezaji na mashabiki wa Liverpool wote walidhani mpira ulikuwa umevuka msitari.
Next Home
ADVERTISMENT
Sanya Consultant Company; deals with project proposal writing, conducting ESIA in different projects, research proposal writing.

contact: +255789606882

LISTEN RADIO FREE AFRICA LIVE

Most viewed Contents

  • TCU Guide book - Kwa wanaoomba vyuo 2012/2013
  • Engaruka:Kabila lililotoweka kimiujiza
  • WASHIRIKI WA BIG BROTHER FROM TANZANIA HAWA HAPA
  • Mbeya
  • Mamba / Marangu
  • MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA 2012/2013
  • MAIGE: "NAPE NI GAMBA"
  • DIAMOND: "NAMSHUKURU WEMA SEPETU KWA KUNIFUNDISHA KIINGEREZA"
  • Boma la Mjerumani Mikindani ni kivutio
  • Bujora Museum

Utalii Tanzania On facebook

football online

Footbal Updates

Get Adobe Flash player
live scores

Online Visiters

© 2012 - Utalii Tanzania. All rights reserved.

Designed by Mhoja L. Matandiko

hit counter