Rais Kagame avunja kimya chake kuhusu tuhuma za DRC dhidi ya Rwanda

 


Rais Paul Kagame wa Rwanda amevunja kimya chake cha muda mrefu kuhusu tuhuma zinazotolewa na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwamba Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na serikali ya Kinshasa Mashariki mwa nchi hiyo na kuitaka DRC kutatua matatizo yake ya ndani badala ya kuwatupia wengine mzigo huo. 

Rais Kagame amewaambia waandishi wa habari kwamba Rwanda ni miongoni mwa nchi zilizoisaidia Congo Kinshasa kurudia hali yake ya kawaida katika miaka ya huko nyuma wakati wa machafuko na haiwezekani tena ikabadili misimamo yake na kuwaunga mkono waasi. 

Amesisitiza kuwa hali mbaya ya usalama katika eneo la mpakani na DRC ni tishio kwa usalama wa nchi yake pia. Hii ni katika hali ambayo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yameituhumu Rwanda kwamba unawaunga mkono waasi wa M23 nayo serikali ya Kinshasa licha ya kutotamka wazi kwamba Rwanda inahusika, lakini imesema inalichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa

0 comments

Leave a Reply