MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA 2012/2013

                               JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
                            Simu: 022-2121600 Faksi: 022-2113271 Tovuti: www.moe.go.tz

  TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

NB: MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kama ifuatavyo:


(A) MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI
1. CHETI DARAJA A: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Aliyehitimu Kidato cha 4 kati ya mwaka 2009 hadi 2011 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa mtihani uliofanyika katika kikao kimoja AU mwenye ufaulu wa masomo manne kwa kiwango cha C au zaidi (masomo yanayofundishwa katika shule za Msingi) kwa mitihani iliyofanyika katika vikao zaidi ya kimoja;


(b) Aliyehitimu Kidato cha 6 na kukosa sifa za kujiunga na Stashahada ni sifa ya nyongeza.
Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry and English‟.


2. CHETI (MICHEZO): MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Ufaulu wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 (Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics, Biology, Physics, Chemistry and English‟;
(b) Aliyehitimu Kidato cha 6 na kukosa sifa za kujiunga na Stashahada ni sifa ya nyongeza; na
(c) Mwenye uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).


3. CHETI (ELIMU YA AWALI): MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Aliyehitimu Kidato cha 4 kati ya mwaka 2009 hadi 2011 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa mtihani uliofanyika katika kikao kimoja; na
(b) Kuhitimu Kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza.


(B) MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA CHETI
1. CHETI SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MWAKA 1
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya ualimu Daraja A;
(b) Uzoefu wa kazi ya ualimu usiopungua miaka 2;
(c) Aliyefaulu masomo ya Sayansi na Sayansi Kimu; na
(d) Aliyefaulu mtihani wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 28.


2. CHETI ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MWAKA 1
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya ualimu Daraja A;
(b) Uzoefu wa kazi ya ualimu usiopungua miaka 2;
(c) Aliyefaulu angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha 4;
(d) Aliyefaulu mtihani wa Kidato cha 4 kwa kiwango kisichopungua daraja la IV alama 28; na
(e) Mwalimu anayefundisha Elimu Maalum hata kama hana mafunzo rasmi ni sifa ya nyongeza(vithibitisho viambatishwe)..


(C) MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA
1. STASHAHADA YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII NA LUGHA : MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha 1 hadi 4.
Masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha 1 hadi 4 ambayo ni; Mathematics, English, Kiswahili, History, Geography, Civics, Biology, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Bookeeping, Commerce.


2. STASHAHADA YA UALIMU MICHEZO, MUZIKI, SANAA ZA UFUNDI NA SANAA ZA MAONESHO: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja kwa kuzingatia masomo yafuatayo kwa kila kozi:
-Sanaa za Ufundi: masomo ya ‘Fine Art’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha 4 masomo ya ‘Biology, History, Physics, English, and Civil Engineering’
-Sanaa za Maonesho: masomo ya ‘Literature in English, Kiswahili, Geography and History;

-Muziki: masomo ya ‘English, Kiswahili, Music, Physics, Geography and History’; na
-Elimu kwa Michezo: masomo ya Biology, Chemistry, Physics, English’ na Kiswahili.


3. STASHAHADA YA UALIMU UFUNDI: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwenye cheti cha FTC kutoka vyuo vya Ufundi (Arusha, Mbeya, Dar es Salaam) au sifa zinazolingana; na
(b) Mwenye umri usiozidi miaka 35.


4. STASHAHADA YA UALIMU KILIMO: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kiwango kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja katika somo la ‘Agricultural’ Science na ‘Biology’ au ‘Chemistry’.


5. STASHAHADA YA UALIMU BIASHARA: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Accounts and Commerce’.


6. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja katika masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.


(D) MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA STASHAHADA
1. STASHAHADA YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII NA LUGHA: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili; na
(b) Ufaulu wa mtihani Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari (Kidato cha 1 hadi 4). Masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari ni; Mathematics, English, Kiswahili, History, Geography, Civics, Biology, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Bookeeping, Commerce.


2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
(b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
(c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).


3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
(b) Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
(c) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.


VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
(i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
(ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
(iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
(iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
(v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
(vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
(vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
(viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

0 comments

Leave a Reply