Wanafunzi wa shule ya sekondari Manow wakiwa chini ya ulinzi wa polisi shuleni hapo |
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela akiwatuliza jazba wanafuzi wa manow |
Haya si makaratasi au takataka bali ni mitihani iliyochanwachanwa na wanafuzi hao |
Wanafunzi wa shule ya Seminary Manow Wilayani Rungwe mkoani Mbeya juzi wamefanya uharibifu wa kuvunja mali ya shule pamoja na kuiba vitu visivyo pungua thamani ya shilingi milion 50.
Akiongea na mwandishi mkuu wa shule hiyo ya Manow Watson Masiba amesema kuwa mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugali baada ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo hakutakuwa na ratiba ya wali kwa kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo stoo,
Uongozi wa shule ulipojitahidi kusuruhisha suala hilo kwa kaandaa chakula hicho usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vulugu kwa kuvunja vioo vya majengo na kuvunja milango na kuiba computa 11 za shule pamoja na kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana mitihani yote iliyo andaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya jana tarehe 15.06.2012.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi na wanakijiji wanao izunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo kwa tofauti kati ya uongozi wa shule na wanafunzi hivyo kufikia wanafunzi hao kutafuta sababu ya kufanya vurugu kwa kiasi cha uharibifu wa mali za shule na kanisa.
akiongea na mwandishi Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema kuwa uharibifu ni mkubwa sana na zaidi ya mali zisizo pungua shilingi milioni 50 zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia pamoja na kuwa uongozi wa shule utawachukulia hatua za kinidham.
Naye mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati yake ya ulinzi na usalama amekemea vikali kitendo kilicho fanywa na wanafunzi hao ukizingatia shule hiyo ni ya kanisa la kiinjili la Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule. Bwana Meela amechukua hatua ya kuifunga shule hiyo hadi tarehe 02.07.2012 kwa kidato cha pili, tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu huo na wanafunzi wajapo shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo binafsi kwa barua. Hadi mwandishi anaondoka hapo jeshi la polisi liliimarisha ulinzi shuleni hapo na wanfunzi 24 walifikishwa police kwa mahojiano zaidi. |
0 comments