Malawi kubatilisha sheria inayozuia mahusiano ya watu wa jinsia moja 5/18/201

Picture


Raia wa Malawi waliotangaza kuoana Steven Monjeza na Tiwonge Chimbalanga, wakiwa kortini mwaka 2010
Jana Ijumaa, katika mwendelezo wa mabadiliko ya uongozi katika nyanja mbalimbali za uongozi wake, Rais wa Malawi, Joyce Banda amesema anataka Serikali yake kubatilisha baadhi ya sheria za nchi hiyo ili kwenda sawa na matakwa ya jamii za Kimataifa, ikiwamo kufuta sheria inayoharamisha ndoa za watu wa jinsia moja na kuwakandamiza.

Rais Banda ameyasema hayo katika hotuba yake ya kwanza iliyo rasmi kwa nchi hiyo, tangu kuingia madarakani mwezi Aprili mwaka huu, baada ya kufariki mtangulizi wake, hayati Rais Bingu wa Mutharika. Banda atashikilia kiti hicho hadi mwaka 2014.
"Indecency and unnatural acts laws shall be repealed" alisema Banda.

Hata hivyo, kubatilisha sheria hiyo kunahitaji kupigiwa kura na Bunge, na hadi sasa Rais Banda anaungwa mkono na Wabunge wengi lakini ni mapema kujua ikiwa wote watapiga kura kwa wingi wa kutosha kuweza kufanikisha mabadiliko hayo.

Ikiwa zoezi hilo litafanikiwa, basi litaifanya Malawi kuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994.

Mwaka 2010, wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana. Baadhi ya makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu na usawa wa kijinsia wa kitaifa na kimataifa walipaza sauti zao na kusababisha baadhi ya nchi za Magharibi, zikiongozwa na Uingereza, kutishia kuinyima baadhi ya misaada ya kiuchumi nchi hiyo kwa kitendo hicho. Hatimaye marehemu Bingu alitangua hukumu ya mahakama na kuwaachilia wawili hao kwa kigezo cha "haki za kibinadamu tu" lakini akasisitiza "bado ni wahalifu dhidi ya mila, desturi, imani na sheria za nchi".

Kwa miaka ya hivi karibuni, baadhi ya viongozi wa nchi wamekuwa wakitishia kutokuzipa misaada ya kiuchumi baadhi ya nchi ambazo hazitatambua haki za watu wenye mahusiano ya jinsia moja.

Tayari baadhi ya wanaharakati wa haki za kibinadamu wamepokea kwa furaha hotuba hiyo lakini wameonyesha wasiwasi wao ikiwa Bunge la nchi hiyo litaridhia uamuzi huo, "The issue of homosexuality has been a contentious issue," amesema Undule Mwakasungula, mmoja wa wanaharakati hao na kuongeza, "Definitely it will raise controversy in parliament."

Huko nchini Afrika Kusini ambayo ni nchi pekee barani Afrika yenye sheria zinazowatambua watu wenye mahusiano ya jinsia moja tangu mwaka 1996, mwanaharakati Mark Heywood anasema Banda atapata uungwaji mkono na jamii ya Kimataifa, ila "I hope that she is persuasive enough in her own country..." "...it's really important for other African countries other than South Africa to move in this direction..." "...symbolically, I think it is very important for Africa."

0 comments

Leave a Reply