MWENGE WA UHURU KUWASHWA LEO KITAIFA MKOANI MBEYA NA WAZIRI MKUU.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), baada ya kumaliza mbio zake mkoani Rukwa.

******
Habari na mwandishi maalum.
Mwenge wa Uhuru utawasha leo kitafa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mgeni Rasmi katika uzinduzi huo wa mbio za mwenge utaongzwa na wazri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
Shughuli hiyo ya uwashawaji wa mwenge utaambatana na uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Sensa ambapo zoezi hilo linatarajia kufanyika Agasti 26 mwaka huu nchini kote.
Kabla ya kuwashwa kwa mwenge huo wa Uhuru watanzania watakao hudhuria tukio hilo muhimu watashuhudia burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya burudani ndani na nje ya mkoa wa Mbeya.
Aidha washiriki watashuhudia watoto wa haraiki wakionesha mambo muhimu ambayo wamefundishwa na wakufunzi wao kwa zaidi ya mizezi mitatu sasa.

0 comments

Leave a Reply